93

Mungu mfalme
1 Mwenyezi-Mungu anatawala; amejivika fahari kuu! Mwenyezi-Mungu amevaa fahari na nguvu! Ameuimarisha ulimwengu, nao hautatikisika kamwe.
2 Kiti chako cha enzi ni imara tangu kale; wewe umekuwapo kabla ya nyakati zote.
3 Vilindi vimetoa sauti, ee Mwenyezi-Mungu; naam, vimepaza sauti yake, vilindi vyapaza tena mvumo wake.
4 Mwenyezi-Mungu ana enzi kuu juu mbinguni, ana nguvu kuliko mlio wa bahari, ana nguvu kuliko mawimbi ya maji.
5 Ee Mwenyezi-Mungu, maagizo yako ni thabiti; nyumba yako ni takatifu milele na milele.

Generic placeholder image