JUMATATU JUMA 12 LA MWAKA WA 1
MASOMO
SOMO 1: Mwa12:1-9
Bwana alimwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende
mpaka nchi nitakayokuonyesha; nami nitakufanya wewe kuwa taifa kubwa, na kukubariki, na kulikuza
jina lako; nawe uwe baraka; nami nitawabariki wakubarikio, naye akulaaniye nitamlaani; na katika
wewe jamaa zote za dunia watabarikiwa. Basi Abramu akaenda, kama Bwana alivyomwamuru; Lutu akaenda
pamoja naye. Naye Abramu alikuwa mtu wa miaka sabini na mitano aiipotoka Harani. Abramu akamchukua
Sarai mkewe, na Lutu mwana wa nduguye, na vitu vyao vyote walivyokuwa wamejipatia, na hao watu
waliowapata huko Harani, wakatoka ili kwenda nchi ya Kanaani; nao wakaingia katika nchi ya Kanaani.
Abramu akapita katikati ya nchi mpaka mahali patakatifu pa Shekemu; mpaka mwaloni wa More. Na
Wakanaani siku zile walikaa katika nchi hiyo. Bwana akamtokea Abramu, akasema, Uzao wako nitawapa
nchi hii. Naye huko akamjengea madhabahu Bwana aliyemtokea. Kisha akaondoka huko akaenda mpaka mlima
ulio upande wa mashariki wa Betheli, akaipiga hema yake; alikuwa na Betheli upande wa magharibi,
na Ai upande wa mashariki; akamjengea Bwana madhabahu huko, akaliitia jina la Bwana. Naye Abramu
akasafiri, akazidi kwenda pandc za kusini.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.33:12-13,18-20,22 (K)12
1. Heri watu aliowachagua kuwa urithi wakc.
Toka mbinguni Bwana huchungulia,
Huwatazama wanadamu wote pia.
(K) Heri taifa ambalo Bwana ni Mungu wao,
watu aliowachagua kuwa urithi wake.
2. Tazama, jicho la Bwana li kwao wamchao,
Wazingojeao faadhili zakc.
Yeye huwaponya nafsi zao na mauti,
Na kuwahuisha wakati wa njaa. (K)
3. Nafsi zetu zinamngoja Bwana;
Yeye ndiyc msaada wetu na ngao yetu.
Ee Bwana, fadhili zako zikae nasi,
Kama vile tulivyokungoja Wewe. (K)
Shangilio: Zab.l9:8
Aleluya, aleluya,
Amri ya Bwana ni sali,
huyatia macho nuru.
Aleluya.
INJILI: Mk.7:1–5
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: Msihukumu msije mkahukumiwa ninyi. Kwa kuwa hukumu mhukumuyo, ndiyo
mtakayohukumiwa; na kipimo kile mpimiacho, ndicho mtakachopimiwa. Basi, mbona wakitazama kibanzi
kilicho ndani ya jicho la ndugu yako, na boriti iliyo ndani ya jicho lako mwenyewe huiangalii? Au
utamwambiaje nduguyo, Niache nikitoe kibanzi katika jicho lako; na kumbe! Mna boriti ndani ya jicho
lako mwenyewe? Mnafiki wewe, itoe kwanza ile boriti katika jicho lako mwenyewe; ndipo utakapoona
vema kukitoa kile kibanzi katika jicho la ndugu yako.
--------------
--------------
MAOMBI
Ndugu, Babu yetu Ibarahimu alifaulu kuishi kwa imani na
utii kwa Mungu. Tunahitaji msaada wa Mungu ili kuiga
mfano huo. Tuombe:-
Kiitikio: Upokee ombi letu.
1. Kwa imani, Ibrahimu alipoitwa aliitika na kwenda
asikokujua. Uwajalie Maaskofu, Mapadre na wote
wenye miito mitakatifu roho ya kimisionari, wapate
kuihubiri Injili kokote unakotaka Wewe. Ee Bwana.
2. Uwaonye watawala wa dunia wasiowaongoza watu
wako kadiri ya sheria na amri zako, ili wageuke na
kuziacha njia zao mbaya. Ee Bwana.
3. Uwajalie watu wote duniani baraka na paji la imani
safi na ya kudumu. Ee Bwana.
4. Utuepushe na unafiki pamoja na utoaji hukumu
tusizostahili kwa jirani zetu. Ee Bwana.
5. Marehemu wetu wapate kibali cha kuingia mbinguni
uliko Wewe. Ee Bwana.
Ee Mungu kwa huruma yako pokea maombi yetu hata
yale ambayo hatukuweza kuyataja. Kwa njia ya Kristo
Bwana wetu. Amina.