JUMANNE JUMA 28 LA MWAKA WA 1
MASOMO

SOMO 1: Rum.1:16-25
Siionei haya Injili; kwa sababu I uweza wa mungu uuletao wokovu, kwa kila aaminiye, kwa Myahudi kwanza, na kwa Myunani pia. Kwa maana haki ya Mung inadhihirishwa ndani yake, toka Imani hata Imani; kama ilivyoandikwa, Mwenye haki ataishi kwa Imani. Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu. Kwa kuwa mambo ya Mungu yanayojulikana yamekuwa Dhahiri ndani yao, kwa maana Mungu aliwadhihirishia. Kwa sababu mambo yake yasiyoonekana tangu kuumbwa ulimwengu yanaonekana, na kufahamika kwa kazi zake; yaani, uweza wake wa milelle na Uungu wake; hata wasiwe na udhuru; kwa sababu, walipomjua Mungu hawakumtukuza kama ndiye Mungu wala kushukuru; bali walipotea katika uzushi wao, na mioyo yao yenye ujinga ikatiwa giza. Wakijinena kuwa wenye hekima walipumbazika; wakaubadili utukufu wa Mungu asiye na uharibifu, na ya ndege, na ya wanyama, na ya vitambaavyo. Kwa ajili ya hayo Mungu aliwaacha katika tamaa za mioyo yao, waufuate uchafu, hata wakavunjiana heshima miili yao. Kwa maana waliibadili kweli ya Mungu kuwa uongo, wakakisujudia kiumbe na kukiabudu badala ya Muumba anayehimidiwa milele. Amina.

WIMBO WA KATIKATI: Zab.19:1-4 (K)1
1. Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu, Na anga laitangaza kazi ya mikono yake. Mchana husemezana na mchana, Usiku hutolea usiku maarifa.

(K) Mbingu zauhubiri utukufu wa Mungu.

2. Hakuna lugha wala maneno, Sauti yao haisikilikani. Sauti yao imeenea duniani mwote, Na maneno yao hata miisho ya ulimwengu. (K)

SHANGILIO: Zab.19:8
Aleluya, aleluya!
Amri ya Bwana ni safi,
huyatia macho nuru.
Aleluya!

INJILI: Lk.11:37-41
Yesu alipokuwa akinena, Farisayo mmoja alimwita aje kwake ale chakula; akaingia, akaketi chakulani. Farisayo huyo alipomwona, alistaajabu kwa sababu hakunawa kabla ya chakula. Bwana akamwambia, Ninyi Mafarisayo mwasafisha kikombe na sahani kwa nje, lakini ndani yenu mmejaa unyang’anyi na uovu. Enyi wapumbavu; aliyevifanya vya nje, siye yeye aliyevifanya vya ndani pia? Lakini, toeni sadaka vile vya ndani, na tazama, vyote huwa safi kwenu.

--------------

--------------
MAOMBI
Ndugu zangu, kwa vile tunategemea ulinzi wa Mungu na malaika wake, tuombe.

Kiitikio: Twakuomba utusikie.
1. Ili Baba Mtakatifu wetu F. na viongozi wote wa Kanisa waone fahari kukudhihirisha Wewe Mungu kwa maneno na matendo. Ee Bwana.

2. Wote waliopotea katika uzushi wajaliwe kurudi katika imani ya kweli, wapate kukutukuza na kuuabudu utukufu wako usio na uharibifu. Ee Bwana.

3. Sisi sote tujaliwe neema ya kutoionea aibu Injili, bali tujibidishe bila udhuru katika kukiri umungu Wako na uweza Wako wa milele. Ee Bwana.

4. Utuepushe na unafiki wa kifarisayo, ili imani yetu ionekane katika matendo ya upendo; na hivyo kutakaswa mwilini na rohoni. Ee Bwana.

5. Ndugu zetu waliofariki dunia wasamehewe dhambi zao na kuuona uso wako mtukufu huko mbinguni. Ee Bwana.

Ee Mungu unayetaka mwenye haki aishi kwa imani, utujalie hayo. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.