JUMAMOSI JUMA 23 LA MWAKA WA 1
MASOMO
SOMO 1: 1Tim.1:15-17
Ni neno la kuaminiwa, tena lastahili kukubalika kabisa, ya kwamba Kristo Yesu alikuja ulimwenguni
awaokoe wenye dhambi; ambao wa kwanza wao ni mimi. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika
katika mimi. Lakini kwa ajili hii nalipata rehema, ili katika mimi wa kwanza, Yesu Kristu audhihirishe
uvumilivu wake wote; niwe kielelezo kwa wale watakaomwamini baadaye, wapate uzima wa milele. Sasa
kwa Mfalme wa milele, asiyeweza kuona uharibifu, asiyeonekana, Mungu peke yake, na iwe heshima na
utukufu, Mungu peke yake, na iwe heshima na utufufu milele na milele.
WIMBO WA KATIKATI: Zab.113:1-7 (K)2
1. Aleluya.
Enyi watumishi wa Bwana, sifuni,
Lisifuni jina la Bwana,
Jina la Bwana lihimidiwe
Tangu leo na hata milele.
(K) Jina la Bwana lihimidiwe tangu leo na hata milele.
2. Toka maawio ya jua hata machweo yake
Jina la Bwana husifiwa.
Bwana ni mkuu juu ya mataifa yote,
Na utukufu wake ni juu ya mbingu. (K)
3. Ni nani aliye mfano wa Bwana,
Mungu wetu aketiye juu;
Anyenyekeaye kutazama,
Mbinguni na duniani?
Humwinua mnyonge kutoka mavumbini,
Na kumpandisha maskini kutoka jaani. (K)
SHANGILIO: Lk.8:15
Aleluya, aleluya!
Wanabarikiwa wale ambao kwa unyofu na wema wa mioyo yao,
hulisikia neno la Mungu na kulishika.
Aleluya.
Aleluya!
INJILI: Lk.6:43-49
Yesu aliwaambia wanafunzi wake: hakuna mti mzuri uzaao matunda mabaya, wala mti mbaya uzaao matunda
mazuri; kwa kuwa kila mti hutambulikana kwa matunda yake; maana, katika miiba hawachumi tini, wala
katika michongoma hawachumi zabibu. Mtu mwema katika hazina njema ya moyo wake hutoa yaliyo mema,
na mtu mwovu katika hazina mbovu ya moyo wake hutoa yaliyo maovu; kwa kuwa mtu, kinywa chake hunena
yale yaujazayo moyo wake. Na kwa nini mnaniita, Bwana, Bwana, walakini hamyatendi nisemayo? Kila
mtu ajaye kwangu, na kuyasikia maneno yangu na kuyatenda, nitawaonesha mfano wake. Mfano wake ni
mtu ajengaye nyumba, na kuchimba chini sana, na kuweka msingi juu ya mwamba; na kulipokuja gharika,
mto uliishukia nyumba ile kwa nguvu, usiweze kuitikisa; kwa kuwa imejengwa vizuri. Lakini yule
aliyesikia ila hakutenda, mfano wake ni mtu aliyejenga nyumba juu ya ardhi pasipokuwa na msingi,
mto ukaishukia kwa nguvu, ikaanguka mara; na maangamizi yake nyumba ile yakawa makubwa.
--------------
--------------
MAOMBI
Wapendwa, Kristo Yesu alikuja kuwaokoa wakosefu
ambao wanatakiwa washirikiane naye katika kuutimiza
ukombozi huo. Kwa maombezi ya Bikira Maria, tusali
tukisema:-
Kiitikio: Upokee ombi letu.
1. Uwasaidie viongozi wetu wa Kanisa kuwa kielelezo
kwa wale wanaokuamini Wewe Mungu, wapate uzima
wa milele. Ee Bwana.
2. Watu wote duniani wakutambue Wewe kuwa ndiwe
Mfalme wa kweli na wa milele, wapate kukuabudu
na kukupa heshima yote. Ee Bwana.
3. Umjalie kila mmoja wetu kulisikiliza neno lako kwa
makini, kulielewa vizuri na kuliishi kwa vitendo, ili
lizae matunda mazuri na ya kudumu. Ee Bwana.
4. Uwaepushe Wakristo na ibada ya sanamu, ili
wasikinywee kikombe cha Bwana na kikombe cha
mashetani; wala kushiriki meza ya Bwana na meza
ya mashetani. Ee Bwana.
5. Ndugu zetu marehemu waliojitahidi kukutafuta kwa
moyo mnyofu wapate tuzo la milele huko mbinguni. Ee Bwana.
Ee Mungu unayetaka tutende unayotuamuru, uyapokee
maombi yetu. Kwa njia ya Kristo Bwana wetu. Amina.