AYUBU 25
A
A

A

<
>




25

Jibu la Bildadi
1 Kisha Bildadi, Mshuhi, akajibu:
2 “Mungu ni mwenye uwezo mkuu, watu wote na wamche. Yeye huweka amani mpaka juu kwake mbinguni.
3 Nani awezaye kuhesabu majeshi yake? Ni nani asiyeangaziwa na mwanga wake?
4 Mtu awezaje basi, kuwa mwadilifu mbele ya Mungu? Binadamu tu awezaje kujidai kuwa safi?

5 Kwake Mungu, hata mwezi haungai vya kutosha; nyota nazo si safi mbele yake;
6 sembuse mtu ambaye ni mdudu, binadamu ambaye ni buu tu!”

Generic placeholder image